14-Jun-12
Watu 74 wanaotuhumiwa kwa kuvamia
mgodi wa ABG North Mara wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga na mishale
kwa nia ya kuiba mawe ya dhababu wamekamatwa na Jeshi la polisi Kanda
Maalum ya TARIME/RORYA.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya TARIME RORYA ACP JUSTUS KAMUGISHA amesema kitendo hicho cha wananchi
kuvamia mgodi ni kosa la jinai na watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa
mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mgodi wa ABG North Mara bado
unaandamwa na uvamizi wa watu wakiwa na silaha za jadi kwa kile kinachodaiwa
kutaka kuiba mawe yanayosemekana kuwa na dhahabu.
Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa
Oparesheni wa Jeshi
la Polisi Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi SIMON SIRRO amesema jeshi
hilo
pamoja na kukamata wavamizi, pia limefanya mazungumzo na viongozi pamoja na wazazi ili kutafuta suruhu ya
kudumu itakayo komesha tatizo la uvamizi wa Mgodi, tatizo ambalo
amekili kuwa ni la muda mrefu na wazazi wasiposhirikishwa katika
kutafuta njia muafaka ya kumaliza mgogoro huu uliopo kati ya wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la mgodi wa ABG North Mara ''Nyamongo'' basi tutegemee hadithi ilele iliyodumu zaidi ya muongo mmoja sasa.
No comments:
Post a Comment