Wednesday, July 11, 2012

*DK. SLAA AZUIWA KUOA*-Rose Kamili Anayedai Kuwa Ni Mke Wa Katibu Mkuu Wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, Amefungua Kesi Mahakama Kuu Akiiomba Isimamishe Ndoa Ya Kiongozi Huyo Na Mke Mwingine Inayotarajiwa Kufungwa Julai 21 Mwaka Huu Wilayani Karatu, Mkoa Wa Manyara. Dk Slaa Anatarajia Kufunga Ndoa Na Mchumba Wake Wa Siku Nyingi, Josephine Mushumbusi. Rose Kamili Mbunge Wa Chadema Pia Anaiomba Mahakama Iamuru Dk. Slaa Amlipe Shs Mil. 50 Za Fidia Aliyotumia Kujihudumia Pasipo Matunzo Ya Mumewe Huyo. Mbunge Huyo Kupitia Kwa Wakili Wake Joseph Thadayo, Anaiomba Pia Mahakama Iamuru Josephine Mushumbusi Amlipe Kiasi Cha Shs Mil. 500 Za Fidia Ya Maumivu Aliyoyapata Kutokana Na Kitendo Chake Cha Kuingilia Ndoa Yao. Kesi Hiyo Namba 4 Ya Mwaka 2012 Iliyopangwa Kusikilizwa Na Jaji Lawrance Kaduli Inatarajia Kutajwa Kwa Mara Ya Kwanza Leo. Katika Hati Hiyo Ya Madai, Mbunge Huyo Anadai Kuwa Ndoa Inayotarajiwa Kufungwa Kati Ya Dk. Slaa Na Josephine Mushumbusi Ni Batili Kwa Sababu Kuna Ndoa Nyingine Halali Na Inayoendelea Kuishi Kati Ya Slaa Na Rose Iliyofungwa Mwaka 1985. Alidai Baada Ya Kufungwa Kwa Ndoa Hiyo Juni 18, 1987 Walifanikiwa Kupata Mtoto Wa Kike Anayeitwa Emiliana Slaa Na Badaye Septemba 23, 1988 Walipata Mtoto Mwingine Wa Kiume Aitwaye Linus Slaa. Katika Uhusiano Wao Dk. Slaa Akiwa Padri Wa Kanisa Katoliki Alifanya Taratibu Za Kujiondoa Katika Nafasi Hiyo Na Kuanza Maisha Ya Familia. TAFAKARI..