Wednesday, August 8, 2012
Wednesday, July 11, 2012
*DK. SLAA AZUIWA KUOA*-Rose Kamili Anayedai Kuwa Ni Mke Wa Katibu Mkuu Wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, Amefungua Kesi Mahakama Kuu Akiiomba Isimamishe Ndoa Ya Kiongozi Huyo Na Mke Mwingine Inayotarajiwa Kufungwa Julai 21 Mwaka Huu Wilayani Karatu, Mkoa Wa Manyara. Dk Slaa Anatarajia Kufunga Ndoa Na Mchumba Wake Wa Siku Nyingi, Josephine Mushumbusi. Rose Kamili Mbunge Wa Chadema Pia Anaiomba Mahakama Iamuru Dk. Slaa Amlipe Shs Mil. 50 Za Fidia Aliyotumia Kujihudumia Pasipo Matunzo Ya Mumewe Huyo. Mbunge Huyo Kupitia Kwa Wakili Wake Joseph Thadayo, Anaiomba Pia Mahakama Iamuru Josephine Mushumbusi Amlipe Kiasi Cha Shs Mil. 500 Za Fidia Ya Maumivu Aliyoyapata Kutokana Na Kitendo Chake Cha Kuingilia Ndoa Yao. Kesi Hiyo Namba 4 Ya Mwaka 2012 Iliyopangwa Kusikilizwa Na Jaji Lawrance Kaduli Inatarajia Kutajwa Kwa Mara Ya Kwanza Leo. Katika Hati Hiyo Ya Madai, Mbunge Huyo Anadai Kuwa Ndoa Inayotarajiwa Kufungwa Kati Ya Dk. Slaa Na Josephine Mushumbusi Ni Batili Kwa Sababu Kuna Ndoa Nyingine Halali Na Inayoendelea Kuishi Kati Ya Slaa Na Rose Iliyofungwa Mwaka 1985. Alidai Baada Ya Kufungwa Kwa Ndoa Hiyo Juni 18, 1987 Walifanikiwa Kupata Mtoto Wa Kike Anayeitwa Emiliana Slaa Na Badaye Septemba 23, 1988 Walipata Mtoto Mwingine Wa Kiume Aitwaye Linus Slaa. Katika Uhusiano Wao Dk. Slaa Akiwa Padri Wa Kanisa Katoliki Alifanya Taratibu Za Kujiondoa Katika Nafasi Hiyo Na Kuanza Maisha Ya Familia. TAFAKARI..
Wednesday, July 4, 2012
Saturday, June 30, 2012
Vyombo vya habari vyatakiwa kuepuka habari za kuchonganisha
Thursday, 19 May 2011 13:30
Vyombo vya habari vimetakiwa kuwa makini na kuepuka kuandika habari
zinazohusu imani za kidini kwa kuegemea upande mmoja ama kwa majumuisho
ili kuepusha kuchochea chuki miongoni mwa jamii.
“ Jambo hilo ni muhimu siyo tu kwa manufaa ya taaluma bali pia kwa kulinda amani na umoja katika Taifa’, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam leo.
Mukajanga, alisema kuwa kumeibuka uandishi usiozingatia uhalisia, ulinganishi na umahususi badala yake uandisi unachukua mfumo wa kuegemea upande mmoja na kufanya majumuisho yasiyotokana na ukweli uliothibitishwa na mwandishi.
“Mapungufu hayo ya kiweledi”, alisema, “yamesababisha habari nyingi kuwa potofu na chonganishi”.
Alisema kuwa weledi hautaki kwa mfano gazeti kumhoji sheikh mmoja au kadhaa au askofu mmoja au kadhaa na kuandika vichwa vya habari vinavyosema “ Waislamu wataka….” au “ Wakristo wakata..”.
“Ikiwa yanayosemwa ni mawazo ya kiongozi mmoja wa dini ni bora isemwe hivyo. Dhehebu linaweza kuhusishwa tu ikiwa yeye ni msemaji rasmi na anaongea kwa niaba ya dhehebu hilo”, alisema Mukajanga.
Vichwa vya habari kama “Maaskofu wamng’oa Naibu Meya Arusha” huku kukiwa `hakuna ushahidi wowote ndani ya habari yenyewe unaoashiria kuwa kujiuzulu kwa huyo Naibu Meya kulitokana na shinikizo la maaskofu ni upotoshaji unaoweza kusababisha chuki, amesema Mukajanga.
Mbaya zaidi, Mukajanga alisema, ni pale kesho yake gazeti jingine linapowatafuta masheikh na kuwaomba kauli yao kuhusiana na kung’olewa kwa Naibu Meya kulikofanywa na maaskofu.
“Ni wazi hapa kuna hatari ya ya wanahabari kugeuka wachonganishi”, alisema Mukajanga.
Pia alisema kumewahi kuchapishwa kichwa kilichosema “ Masheikh wawaonya maaskofu”. Hii ni hatari, alisema.
Mukajanga pia alisema habari nyingine ilidai bila uthibitisho wowote kuwa waumini wa Kanisa Katoliki wametengwa na Kanisa hilo kwa kujihusisha na chama fulani cha siasa. Viongozi wa kanisa hilo hawakuhojiwa, alisema.
Hivi karibuni, Mukajanga alisema, gazeti moja liliandika “Waislamu: Osama hajafa – wadai kuzikwa haraka ni dalili za kuficha ukweli”.
Mukajanga alihoji hivi ni kweli maoni kwamba Osama hajafa yalikuwa maoni ya waislamu wote nchini?
Pia aliuliza baada ya Al-Qaeda wenyewe kukiri kuwa Osama kafa, gazeti hilo halikusikia vibaya kwamba limewasababishia dhihaka Waislamu wote bila uhalali wowote lilipowasingizia kwamba wamesema Osama hajafa?
Gazeti lingine, Mukajanga alisema lilimnukuu mchungaji mmoja aliyepinga ukaguzi wa mahesabu ya makanisa na kuandika kichwa cha habari kilichosema “Makanisa yakataa kukagulkiwa na serikali”.
Hata hivyo Mukajanga alisema, baadaye katibu wa makanisa hayo yaliyotajwa alinukuliwa akisisitiza kuwa yale yalikuwa mawazo binafsi ya mchungaji huyo.
Mukajanga alinukuu kifungu cha 1.9 cha kanuni za maadili kwa wahariri (uk5) kuzuia ubaguzi kinachosisitiza: Hakikisha habari hazilengi wala kutoa nafasi kwa ubaguzi wa kijinsia, dini makundi ya watu wachache, umri, kabila…”
Kuhusu dini , alisema, kifungu 1.14 (uk6) kinaelekeza: Zungumza na mashrikia ya dini, yape haki sawa na heshima yanayostahili kwani hadhi za wawakilishi, viongozi, waumini na imani zao zinapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa.
mwisho

Saturday, June 16, 2012
JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU TARIME RORYA LAKAMATA WATU 74 WANAODAIWA KUVAMIA MGODI WA DHAHABU NYAMONGO ABG.
14-Jun-12
Watu 74 wanaotuhumiwa kwa kuvamia
mgodi wa ABG North Mara wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga na mishale
kwa nia ya kuiba mawe ya dhababu wamekamatwa na Jeshi la polisi Kanda
Maalum ya TARIME/RORYA.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya TARIME RORYA ACP JUSTUS KAMUGISHA amesema kitendo hicho cha wananchi
kuvamia mgodi ni kosa la jinai na watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa
mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mgodi wa ABG North Mara bado
unaandamwa na uvamizi wa watu wakiwa na silaha za jadi kwa kile kinachodaiwa
kutaka kuiba mawe yanayosemekana kuwa na dhahabu.
Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa
Oparesheni wa Jeshi
la Polisi Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi SIMON SIRRO amesema jeshi
hilo
pamoja na kukamata wavamizi, pia limefanya mazungumzo na viongozi pamoja na wazazi ili kutafuta suruhu ya
kudumu itakayo komesha tatizo la uvamizi wa Mgodi, tatizo ambalo
amekili kuwa ni la muda mrefu na wazazi wasiposhirikishwa katika
kutafuta njia muafaka ya kumaliza mgogoro huu uliopo kati ya wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la mgodi wa ABG North Mara ''Nyamongo'' basi tutegemee hadithi ilele iliyodumu zaidi ya muongo mmoja sasa.
AJALI MBAYA YA WAPANDA PIKIPIKI "BODABODA "MUSOMA.
Watu watatu akiwemo mwanamke mmoja anayekadiriwa KUWA na umri kati ya miaka 70 na 75 wamepata ajali mbaya katika balabala ya Mukendo mjini Musoma baada ya pikipiki hizo kugongana uso kwa uso. inadaiwa.
Mashuhuda wa ajali hiyo anadai chanzo cha ajali ni mwendo wa kasi na kutozingatia matumizi sahihi ya alama za Balabalani.Majeruhi wote wamekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Mara mjini hapa, hali za majeruhi ni mbaya.
Tatizo la waendesha Bodaboda kutozingatia sheria za usalama barabarani na alama za barabarani limekua ni tatizo sugu na lisipodhibitiwa vikamilifu litasababisha vifu vingi.
Mashuda wa ajali hii wanawalalamikia mno Madereva wa BODABODA kwa madai kuwa wengi wao hawana Elimu ya matumizi ya Barabara na Udereva.
Friday, June 15, 2012
MANDHARI MURUWA YA BWALO LA POLISI MARA.
Uzuri wa ufukwe huu wanaojivunia watu wa Musoma ni matunda waliyoyavuna toka kwa kamanda Mwadilifu mpendwa wa watu ACP BOAZ aliyehamia kikazi mkoa wa Kilimanjaro hakika anapongezwa kwa mengi zaidi ni ukarabati mkubwa alioufanya katika Bwalo la Maofisa wa polisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)