Saturday, June 30, 2012

Vyombo vya habari vyatakiwa kuepuka habari za kuchonganisha

Vyombo vya habari vimetakiwa kuwa makini na kuepuka kuandika habari zinazohusu imani za kidini kwa kuegemea upande mmoja ama  kwa majumuisho ili kuepusha  kuchochea chuki miongoni mwa jamii.
“ Jambo hilo ni muhimu siyo tu  kwa manufaa ya taaluma  bali pia  kwa kulinda amani na umoja  katika Taifa’, Katibu Mtendaji  wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga aliwaambia waandishi wa habari  mjini Dar es Salaam leo.
Mukajanga, alisema kuwa kumeibuka  uandishi  usiozingatia  uhalisia, ulinganishi na umahususi badala yake  uandisi unachukua mfumo wa kuegemea upande mmoja  na kufanya majumuisho yasiyotokana na  ukweli uliothibitishwa na mwandishi.
“Mapungufu hayo ya kiweledi”, alisema, “yamesababisha habari nyingi kuwa potofu na chonganishi”.
Alisema kuwa weledi hautaki  kwa mfano gazeti kumhoji sheikh mmoja au kadhaa au askofu mmoja au kadhaa na kuandika  vichwa vya  habari vinavyosema “ Waislamu wataka….” au “ Wakristo wakata..”.
“Ikiwa yanayosemwa ni mawazo ya kiongozi mmoja wa dini ni bora isemwe hivyo. Dhehebu linaweza kuhusishwa  tu ikiwa  yeye ni msemaji rasmi na anaongea kwa niaba ya dhehebu hilo”,  alisema Mukajanga.
Vichwa vya habari kama “Maaskofu wamng’oa Naibu Meya Arusha” huku kukiwa `hakuna ushahidi wowote ndani ya habari yenyewe unaoashiria kuwa  kujiuzulu kwa  huyo Naibu Meya  kulitokana na shinikizo la maaskofu ni upotoshaji unaoweza kusababisha chuki, amesema Mukajanga.
Mbaya zaidi, Mukajanga alisema,  ni pale  kesho yake gazeti jingine  linapowatafuta masheikh  na kuwaomba kauli  yao kuhusiana na  kung’olewa kwa Naibu Meya kulikofanywa na  maaskofu.
“Ni wazi hapa kuna hatari ya  ya wanahabari kugeuka wachonganishi”, alisema Mukajanga.
Pia  alisema kumewahi kuchapishwa kichwa kilichosema “ Masheikh wawaonya maaskofu”. Hii ni hatari,  alisema.
Mukajanga pia  alisema  habari nyingine ilidai bila  uthibitisho wowote kuwa waumini wa Kanisa Katoliki wametengwa na Kanisa hilo kwa kujihusisha na chama fulani cha siasa. Viongozi wa kanisa  hilo hawakuhojiwa, alisema.
Hivi karibuni, Mukajanga  alisema, gazeti moja liliandika “Waislamu: Osama hajafa – wadai kuzikwa haraka ni  dalili za kuficha ukweli”.
Mukajanga alihoji hivi ni  kweli maoni kwamba Osama  hajafa yalikuwa maoni ya waislamu wote nchini?
Pia aliuliza baada ya  Al-Qaeda wenyewe  kukiri kuwa Osama kafa, gazeti hilo  halikusikia vibaya kwamba limewasababishia dhihaka Waislamu wote bila uhalali wowote lilipowasingizia kwamba wamesema Osama hajafa?
Gazeti lingine, Mukajanga alisema lilimnukuu mchungaji mmoja  aliyepinga  ukaguzi wa mahesabu  ya makanisa na kuandika  kichwa cha habari  kilichosema “Makanisa yakataa kukagulkiwa na serikali”.
Hata hivyo  Mukajanga alisema, baadaye  katibu wa makanisa hayo  yaliyotajwa  alinukuliwa akisisitiza kuwa yale yalikuwa mawazo binafsi ya mchungaji huyo.
Mukajanga alinukuu kifungu cha  1.9 cha kanuni za  maadili kwa wahariri (uk5) kuzuia ubaguzi kinachosisitiza: Hakikisha  habari hazilengi  wala kutoa nafasi kwa ubaguzi wa kijinsia, dini makundi ya watu wachache, umri, kabila…”
Kuhusu dini , alisema, kifungu 1.14 (uk6) kinaelekeza: Zungumza na mashrikia  ya dini, yape haki sawa na heshima yanayostahili kwani hadhi za wawakilishi, viongozi, waumini na imani zao zinapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa.
mwisho

Saturday, June 16, 2012

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU TARIME RORYA LAKAMATA WATU 74 WANAODAIWA KUVAMIA MGODI WA DHAHABU NYAMONGO ABG.


14-Jun-12                                  

 Watu  74 wanaotuhumiwa kwa  kuvamia  mgodi wa ABG North Mara wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga na mishale kwa nia ya kuiba mawe ya dhababu wamekamatwa na Jeshi la polisi   Kanda Maalum ya TARIME/RORYA.

 Kamanda wa polisi kanda maalumu ya TARIME RORYA ACP JUSTUS KAMUGISHA amesema kitendo hicho cha wananchi kuvamia mgodi ni kosa la jinai na watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mgodi wa ABG North Mara bado unaandamwa na uvamizi wa watu wakiwa na silaha za jadi kwa kile kinachodaiwa kutaka kuiba mawe yanayosemekana kuwa na dhahabu.


Akiongea na waandishi wa Habari Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi SIMON SIRRO amesema jeshi hilo pamoja na kukamata wavamizi, pia limefanya mazungumzo na viongozi pamoja na wazazi ili kutafuta suruhu ya kudumu itakayo komesha tatizo la uvamizi wa Mgodi,  tatizo ambalo amekili kuwa ni la muda mrefu na wazazi wasiposhirikishwa katika kutafuta njia muafaka ya kumaliza mgogoro huu uliopo kati ya wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la mgodi wa ABG North Mara ''Nyamongo'' basi tutegemee hadithi ilele iliyodumu zaidi ya muongo mmoja sasa.








AJALI MBAYA YA WAPANDA PIKIPIKI "BODABODA "MUSOMA.





Watu watatu akiwemo mwanamke mmoja anayekadiriwa KUWA na umri kati ya miaka 70 na 75   wamepata ajali mbaya katika balabala ya Mukendo  mjini Musoma  baada ya pikipiki hizo kugongana uso kwa uso. inadaiwa.
Mashuhuda wa ajali hiyo anadai chanzo cha ajali  ni mwendo wa kasi na kutozingatia matumizi sahihi ya alama za Balabalani.Majeruhi wote wamekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Mara mjini hapa, hali za majeruhi ni mbaya.
Tatizo la waendesha Bodaboda kutozingatia sheria za usalama barabarani na alama za barabarani limekua ni tatizo sugu na lisipodhibitiwa vikamilifu litasababisha vifu vingi.
Mashuda wa ajali hii wanawalalamikia mno Madereva wa BODABODA kwa madai kuwa wengi wao hawana Elimu ya matumizi ya Barabara na Udereva.

Friday, June 15, 2012

MANDHARI MURUWA YA BWALO LA POLISI MARA.

Uzuri wa ufukwe huu wanaojivunia watu wa Musoma ni matunda waliyoyavuna toka kwa kamanda Mwadilifu mpendwa wa watu ACP BOAZ aliyehamia kikazi mkoa wa Kilimanjaro hakika anapongezwa kwa mengi zaidi ni ukarabati mkubwa alioufanya katika Bwalo la Maofisa wa polisi.